Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Miongoni mwa Aayah zilizothibiti kuhusu sifa ni pamoja na maneno Yake Allaah (´Azza wa Jall):

كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ

”Kila aliyekuwa humo [mbinguni na ardhini] atatoweka. Na utabakia uso wa Mola Wako wenye utukufu na wenye ukarimu.”[1]

MAELEZO

Sifa zilizotajwa na mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) miongini mwa sifa za Allaah. Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) ametaja baadhi ya sifa za Allaah. Nitazizungumzia kwa mujibu wa mpangilio wa mtunzi.

1 – Uso. Uso umethibiti kwa Allaah (Ta´ala) kwa dalili ya Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya Salaf. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ

”Utabakia uso wa Mola wako.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Sa´d bin Abiy Waqqaas:

“Hakika wewe hutotoa matumizi yoyote hali ya kuwa ni mwenye kutaka uso wa Allaah isipokuwa utalipwa kwayo.”[3]

Kuna maafikiano juu yake.

Salaf wameafikiana juu ya kumthibitishia Allaah (Ta´ala) uso. Kwa hiyo ni lazima kumthibitishia nao pasi na kupotosha, kukanusha, kuufanyia namna wala kuupigia mfano. Ni uso wa ukweli unaolingana na Allaah.

Ahl-ut-Ta´twiyl wamefasiri kuwa ni thawabu. Tunawaraddi kwa yale yaliyokwishatangulia katika kanuni ya nne.

[1] 55:26-27

[2] 55:27

[3] al-Bukhaariy (1295) na Muslim (1628).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 48
  • Imechapishwa: 17/10/2022