Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

47 – Kila mmoja amewepesishiwa kwa kile alichoumbiwa.

MAELEZO

Ni sehemu ya Hadiyth ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) aliyoipokea al-Bukhaariy na Muslim. Nimeikagua katika “Dhwilaal-ul-Jannah fiy Takhriyj-is-Sunnah” (171). Imesihi kwamba pindi baadhi ya Maswahabah walipomsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anazungumza namna hiyo, walisema:

”Basi tunapambana.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

” Hivi sasa tunapambana, hivi sasa tunapambana, hivi sasa tunapambana.”[1]

Ni Radd ya wazi kabisa kwa Jabriyyah wanaodai kuwa wanategemea makadirio kikamilifu. Wanaifahamu Hadiyth kinyume kabisa na walivyofahamu Maswahabah.

[1] “Dhwilaal-ul-Jannah fiy Takhriyj-is-Sunnah” (161) na (167).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 40
  • Imechapishwa: 23/09/2024