Imaam Abu Bakr al-Bayhaqiy amesema:

”Mlango kuhusu Kulingana juu. Allaah (Ta´ala) amesema:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi.”[2]

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ

“Naye  ni Mwenye kutenza nguvu juu ya waja Wake.”[3]

يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ

“Wanamkhofu Mola wao Aliye juu yao na wanafanya yale wanayoamrishwa.”[4]

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake linapanda neno zuri na tendo zuri hulitukuza.”[5]

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

“Je, mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika? Au mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokutumieni tufani ya mawe basi mtajua vipi maonyo Yangu.”[6]

Kwa maana juu ya mbingu, kama Aayah isemayo:

وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ فِي جُذُوعِ النَّخْلِ

“Nitakusulubuni katika (فِي) mashina ya mitende.”[7]

Bi maana juu ya mashina ya mitende.

فَسِيحُوا فِي الْأَرْضِ

“Basi tembeeni katika (فِي) ardhi… ”[8]

Bi maana juu ya ardhi. Kila kilicho juu huitwa mbingu. ´Arshi ndiyo ya juu ya mbingu zote. Kwa hiyo maana ya Aayah ni kuwa Yule ambaye yuko juu ya mbingu, kama alivyotamka wazi katika Aayah nyinginezo. Katika Aayah hizi tulizozitaja kuna dalili ya kubatilisha madai ya wale miongoni mwa Jahmiyyah wanaosema kuwa Allaah kwa dhati Yake yupo kila mahali. Kuhusiana na Aayah isemayo:

وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ

“Naye yupamoja nanyi popote mlipo..”[9],

makusudio ni kwa ujuzi Wake na si kwa dhati Yake.”[10]

[1] 20:5

[2] 7:54

[3] 6:61

[4] 16:50

[5] 35:10

[6] 67:16-17

[7] 20:71

[8] 9:2

[9] 57:4

[10] Kitaab-ul-I´tiqaad, uk. 112-115.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 82-83
  • Imechapishwa: 29/12/2025