Tafsiri ya Ibn ‘Atwiyyah na mfano wake zinaafikiana zaidi na Sunnah na Mkusanyiko na kusalimika kutokamana na Bid´ah kuliko tafsiri ya az-Zamakhshariy. Ingelikuwa bora na jambo la kupendeza zaidi kama angelinukuu maneno ya Salaf yaliyopo kwenye tafsiri zilizopokelewa kutoka kwao. Mara nyingi hunukuu kutoka kwenye tafsiri ya Muhammad bin Jariyr at-Twabariy, ambayo ni miongoni mwa tafsiri za thamani kubwa na zenye nafasi ya juu zaidi, sambamba na hilo anayaacha yale aliyoyanukuu Ibn Jariyr kutoka kwa Salaf – pasi na kutaja chochote kabisa. Badala yake hutaja, kutokana na anavyodai yeye, kwamba ndio maoni ya wahakiki. Hakika si vyenginevyo wakusudiwa huwa ni kundi la wanafalsfa ambao wameithibitisha misingi yao kutokana na misingi ya Mu´tazilah, ingawa wao wako karibu zaidi na Sunnah kuliko Mu’tazilah. Hata hivyo kila mmoja alitakiwa ampe haki yake na ieleweke kuwa hii ni miongoni mwa tafsiri tegemezi katika madhehebu. Kwa sababu Maswahabah, wanafunzi wao na maimamu wakitafsiri Aayah kadhaa kwa njia fulani na wakaja watu wengine kufasiri Aayah hiyohiyo kwa njia nyingine kutokana na ´Aqiydah wanayoamini, ambayo siyo miongoni mwa ´Aqiydah za Maswahabah na wanafunzi wao, basi wanakuwa wameshirikiana na Mu´tazilah na watu wa Bid´ah wengine katika jambo hili. Yeyote anayepuuza madhehebu ya Maswahabah na wanafunzi wao na akaenda katika tafsiri inayopingana nao, si kwamba amekosea peke yake, bali pia ni mzushi ijapokuwa ni Mujtahid ambaye kosa lake linasamehewa.
Lengo ni kufafanua njia za elimu, dalili zake na njia za kufikia usahihi. Tunajua kuwa Qur-aan ilisomwa na Maswahabah, wanafunzi wao na wale waliokuja baada ya hapo. Tunatambua ya kwamba wao walikuwa ni wajuzi zaidi wa tafsiri yake na maana zake, kama jinsi walikuwa wajuzi zaidi wa haki ambayo Allaah amemtumiliza kwayo Mtume Wake (Swalla Allahu Alayhi Wasallam). Hivyo basi yeyote anayeenda kinyume na maono yao na akaifasiri Qur-aan kinyume na tafsiri yao, basi amekosea katika dalili na kile anachokitolea dalili. Hapana shaka kwamba kila anayepingana na maono yao anayo shubuha fulani anayoitaja, ima iwe ni ya kiakili au ya kiwahy, kama ilivyoelezwa kwa kina katika maeneo mengine.
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 80-82
- Imechapishwa: 07/04/2025

Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 80-82
Imechapishwa: 07/04/2025
https://firqatunnajia.com/24-tafsiri-nyingine-isiyokuwa-ya-maswahabah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket