Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya kurejea ni Kauli Yake (Ta´ala):

وَأَنِيبُوا إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُوا لَهُ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَكُمُ الْعَذَابُ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ

“Rejeeni kwa Mola wenu na jisalimisheni Kwake kabla haijakufikieni adhabu kisha hamtonusuriwa.” (39:54)

MAELEZO

Vilevile kurejea ni ´ibaadah. Amesema (Ta´ala):

وَأَنِيبُوا إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُوا لَهُ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَكُمُ الْعَذَابُ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ

“Rejeeni kwa Mola wenu na jisalimisheni Kwake kabla haijakufikieni adhabu kisha hamtonusuriwa.” (39:54)

Kurejea maana yake ni kutubia kwa Allaah na kumtii. Hii ni ´ibaadah anayofanyiwa Allaah. Ni wajibu kwa watu kurejea kwa Allaah, kutubia Kwake na kumtii.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 35
  • Imechapishwa: 21/12/2016