Swali: Kuna mtu alitaka kumjamii mke wake mchana wa Ramadhaan. Hivyo akalazimika kufungua kwa makusudi ili apate kumwingilia mke wake pasi na yeye kuridhia. Ni kipi kinachowalazimu?

Jibu: Amefanya dhambi kwa njia mbili:

1 – Amefungua kwa makusudi. Kukusudia kufungua katika Ramadhaan ni dhambi na ni moja katika madhambi makubwa. Imepokelewa kwamba:

“Yule mwenye kufungua siku moja ya Ramadhaan pasi na udhuru, basi hawezi kuilipa ijapo atafunga mwaka mzima.”[1]

2 – Amekiuka utukufu wa mwezi kwa jimaa. Kufanya jimaa katika mchana wa Ramadhaan ni dhambi. Kwa hiyo ni analazimika kutubia kwa Allaah kwa sababu ya kufungua swawm yake kwa makusudi. Aidha analazimika kutubia kwa Allaah kwa kufanya kwake jimaa mchana wa Ramadhaan. Vilevile analazimika kutoa kafara nzito kwa kuacha mtumwa huru, asipopata au kile kinacholingana na thamani ya mtumwa, basi atafunga miezi miwili kamilifu na mfululizo juu ya kila siku ambayo alifanya jimaa mchana wa Ramadhaan. Hatokimbilia kulisha chakula isipokuwa akishindwa kufunga kutokana na maradhi au utuuzima. Muda wa kuwa anaweza kufunga basi Allaah hatompa udhuru. Bali atalazimika kufunga miezi miwili mfululizo kama kafara juu ya siku hiyo. Pamoja na kutubia kwa Allaah na kuilipa siku hiyo na asirudi kufanya kitendo kama hicho huko mbeleni. Ikiwa mke wake alilazimishwa na akajaribu kumzuia lakini akamshinda, basi nataraji kuwa itamtosha kufunga siku hiyo.

[1] Ahmad (9705), at-Tirmidhiy (723), Abu Daawuud (2396), Ibn Maajah (1672) na ad-Daarimiy (1756).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 28/03/2022