Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

13 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuunganisha swawm ambapo bwana mmoja katika waislamu akasema: “Hakika wewe unafunga kwa kuunganisha, ee Mtume wa Allaah.” Akasema: “Ni nani katika yenu ambaye ni mfano wangu? Mimi hulala nikilishwa na kunyweshwa na Mola wangu.” Walipokataa kuacha kuunganisha swawm akaunganisha kufunga siku mbili mfululizo kisha wakaona mwezi mwandamo ambapo akasema: “Lau mwezi mwandamo ungelichelewa basi ningekuzidishieni.” Bi maana kwa njia ya kuwakaripia kwa vile walikataa kukoma kuunganisha.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Hadiyth ni dalili kuwa kuunganisha swawm ni ni jambo lililokatazwa. Hekima ya kukatazwa kwake ni madhara yanayoweza kutokea au yanayotarajiwa, kuchosha mwili, kusababisha kuchoka na kupoteza msukumo na kuhatarisha kutotekeleza ipasavyo baadhi ya wajibu wa kidini kama vile kukamilisha swalah, kusoma Qur-aan kwa wingi au majukumu mengine ya kila siku aliyowekewa mwanadamu.

[1] al-Bukhaariy (1965) na Muslim (1103).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/34-35)
  • Imechapishwa: 10/02/2025