Miongoni mwa maajabu ya dhuluma na uonevu wa waandishi hawa ni kuwa, licha ya kuwa wao ndio waliomsingizia kiongozi wa waumini kuzusha, kitu ambacho nimekibainisha, wametushutumu sisi pia kuwa tumemweleza kwa Bid´ah. Pili ni kwamba wameandika matamshi m-balimbali kuhusu hili, mojawapo tumelinukuu na kuliraddi katika kijitabu cha kwanza, uk. 8-9, na kwa ajili hiyo hakuna haja ya kuyarudia hapa. Wala hawakutosheka na tuhuma hii ya uongo, bali wakaongeza jambo kubwa zaidi kwa namna ya kwamba batili ya kwanza ikaonekana kuwa ni ndogo; wamedai kwa uwongo kuwa tumemlaani ‘Umar (Radhiya Allaahu ´anh) – na tunajikinga kwa Allaah na hilo na hata jambo dogo kuliko hilo! Bali wamezidisha zaidi na kutushutumu kwa kuwalaani Salaf wote kwa jumla. Wamedai katika ukurasa wa 10:
“Ewe mwenye kuwatia upotofuni Salaf!”
Wakasema katika ukurasa wa 8:
”Wamewalaani wa mwanzo wa ummah huu na wa mwisho wake!”
Sijapata kuona wenye ujasiri mkubwa wa kuwatuhumu watu wasio na hatia kama hawa. Allaah awarekebishe na awaongoze katika njia iliyonyooka. Na hali yetu nao ni kama alivyosema mshairi:
Mwingine ametenda dhambi, lakini mimi ndiye niliyeadhibiwa –
ni kama kidole cha kushutumu cha mwenye kujuta
Maneno mengine bora zaidi ya mshairi mwengine:
Umenibebesha dhambi ya mtu mwingine na ukamwacha,
Ni kama mwenye ugonjwa wa ukurutu anayeunguza mwingine ilhali yeye yupo salama
Kijitabu chetu hiki kina sura nane:
1 – Mapendezo ya kuswali Tarawiyh kwa mkusanyiko.
2 – Mtume hakuwahi kuswali Tarawiyh zaidi ya Rak´ah kumi na moja.
3 – Kujikita kwake katika Rak´ah kumi na moja ni dalili ya kutofaa kuzidisha juu yake.
4 – ‘Umar aliihuisha Sunnah ya kuswali Tarawiyh kwa mkusanyiko na akaamuru Rak´ah kumi na moja.
5 – Haikuthibiti kuwa kuna Swahabah yeyote ambaye aliswali Tarawiyh Rak´ah ishirini.
6 – Ulazima wa kushikamana na Rak´ah kumi na moja na dalili juu ya hilo.
7 – Namna mbalimbali ambazo Mtume aliswali Witr.
8 – Mahimizo ya kuswali vizuri na matahadharisho ya kuswali vibaya.
Katika maudhui haya kuna sura zingine kama tanzu, faida zingine za Fiqh na Hadiyth na mengineyo ambayo atayapitia msomaji mpendwa. Namuomba Allaah aniwafikishe kuisibu haki katika nilichoandika hapa na katika mengineyo, akifanye kuwa takasifu kwa ajili Yake na awanufaishe kwacho ndugu zangu waumini – kwani hakika Yeye ni Mzuri, Mwenye kurehemu.
Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
1377-09-04 – Dameski
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swalaat-ul-´Iydayn, uk. 7-9
- Imechapishwa: 10/02/2025

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swalaat-ul-´Iydayn, uk. 7-9
Imechapishwa: 10/02/2025
https://firqatunnajia.com/05-sura-za-kitabu-swalaat-ut-taraawiyh/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)