Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya waja wema ni maneno Yake (Ta´ala):

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ

“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta kwa Mola wao njia [na] kumkurubia kadri wanavyoweza na wanataraji rehema Zake na wanakhofu adhabu Yake.”[1]

MAELEZO

Dalili ya kwamba walikuweko ambao wanawaabudu waja wema ni maneno Yake (Ta´ala):

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ

“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta kwa Mola wao njia [na] kumkurubia kadri wanavyoweza na wanataraji rehema Zake na wanakhofu adhabu Yake.”

Bi maana wale ambao mnawaomba badala ya Allaah wanatafuta ukaribu ambako ni kule kujikurubisha kwa Allaah kwa kumtii. Kwa maana nyingine waja wema hawa mnaowaomba wanatafuta ukaribu kwa Allaah kwa kumtii. Vipi basi mtawaabudu ilihali wao wenyewe wanamwabudu Allaah na wanatafuta ukaribu kutoka kwao ilihali waja wema wanajikurubisha mbele ya Allaah?

Kuna maoni yanayosema kuwa Aayah hii imeteremka juu ya watu ambao walikuwa wakiabudia majini baadaye majini hayo yakasilimu. Matokeo yake wale waliokuwa wakiwaabudu wakabaki katika shirki yao na hawakujua kuwa wamesilimu. Ndipo Allaah akawakhabarisha kwamba wale wawaombao ni wapwekeshaji na nyinyi mmebaki katika shirki zenu. Wale muwaombao wamekwishasilimu, enyi watu washirikina[2].

Njia na ukatikati (الوسيلة) maana yake ni ukaribu. Kwa maana nyingine wanatafuta ukaribu kwa Allaah kwa kumtii.

[1] 17:57

[2] Tazama ”Swahiyh-ul-Bukhaariy” (4346) na Tafsiyr ya Ibn Kathiyr (05/88).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 145
  • Imechapishwa: 12/03/2023