Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

… dini yake…

MAELEZO

Kujua msingi wa pili ambao ni dini yake ambayo amekalifishwa kuitendea kazi na ile hekima, rehema na manufaa yote ambayo yanamwelekeza kiumbe kwayo na madhara yote ambayo inamkinga nayo.

Yule mwenye kuzingatia juu ya dini ya Uislamu kwa njia ya usawa mazingatio yaliyojengeka juu ya Qur-aan na Sunnah, basi atatambua kuwa Uislamu ndio dini ya haki ambayo manufaa ya viumbe hayawezi kutekelezeka isipokuwa kwayo. Hata hivyo haitakikani kulinganisha Uislamu na hali ya waislamu hii leo. Hakika ya waislamu wamepuuza mambo mengi na kujiingiza ndani ya madhambi makubwa. Hali imefikia kiasi cha kwamba baadhi ya miji yule anayeishi baina yao kana kwamba anaishi katika jamii isiyokuwa ya Kiislamu.

Dini ya Uislamu – kwa himdi za Allaah – ina manufaa yote ambayo dini zilizotangulia ilikuwa nayo. Kile ambacho Uislamu unatofautiana nazo ni kwamba ni nzuri na yenye kusilihi na inatumika katika kila zama, mahali na kwa watu wote. Maana ya kwamba ni yenye kusilihi kwa watu wote na kila zama ni kwamba kushikamana nayo hakupingani na manufaa ya Ummah katika kila wakati na kila mahali. Kwa hiyo Uislamu unaita katika kila tendo jema na kukataza kila tendo baya. Inaita katika kila tabia nzuri na kukataza kila tabia mbaya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 44-45
  • Imechapishwa: 20/05/2020