Swali 23: Je, swalah ya ijumaa inayo Sunnah kabla au baada yake?

Jibu: Swalah ya ijumaa haina Raatibah kabla yake kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Lakini imesuniwa kwa muislamu anapofika msikitini akaswali kile ambacho Allaah amemuwepesishia katika Rak´ah ambapo ataleta Tasliym kila baada ya Rak´ah mbili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah ya usiku na mchana ni Rak´ah mbilimbili.”[1]

Ameipokea Imaam Ahmad na watunzi wa nne wa Sunan kwa cheni ya wapokezi ilio nzuri. Msingi wake uko katika “as-Swahiyh” pasi na kutaja mchana.

Isitoshe imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth nyingi yanayofahamisha kwamba kilichowekwa katika Shari´ah kwa muislamu pindi anapofika msikitini siku ya ijumaa basi aswali kile ambacho Allaah amemwandikia kabla ya imamu kujitokeza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuweka katika hilo kikomo cha Rak´ah maalum. Akiswali Rak´ah mbili, nne au zaidi ya hizo yote ni mazuri. Uchache wa hayo ni zile Rak´ah mbili za mamkuzi ya msikiti.

Kuhusu baada yake kuna Sunnah Raatibah. Uchache wake ni Rak´ah mbili na wingi wake ni Rak´ah nne. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote katika nyinyi mwenye [kutaka] kuswali baada ya ijumaa, basi aswali baada yake [Rak´ah] nne.”[2]

Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiswali Rak´ah mbili baada ya ijumaa nyumbani kwake.

[1] at-Tirmidhiy (597) na Ibn Maajah (1322).

[2] Muslim (881), at-Tirmidhiy (481) na ad-Daarimiy (1575) na tamko ni lake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 63-64
  • Imechapishwa: 28/11/2021