Swali 23: Tunataraji utatutajia baadhi ya vitabu vya Salafiyyah ambavyo vijana Salafiyyuun wanatakiwa kuvitilia umuhimu na kuviweka katika Maktabah za majumbani mwao?
Jibu: Vitabu ambavyo mwanafunzi anatakiwa kuvitilia umuhimu ni vya Hadiyth kama mfano wa vile vitabu vya Sunan sita; al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy, Ibn Maajah na “al-Musnad” ya Imaam Ahmad. Kadhalika “Swahiyh Jaami´ as-Swaghiyr” na nyongeza yake ya al-Albaaniy, “Silsilah Ahaadiyh as-Swahiyhah” ya al-Albaaniy. Vilevile vitabu vya Muhaddithuun waliotangulia kama vya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na wanachuoni waliokuwepo zama zake na baada ya zama zake. Pia vitabu vya Salafiyyuun waliyopo hii leo kama Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz, Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdullaah Aalus-Shaykh, Shaykh ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan, Shaykh Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan na Shaykh Swaalih al-Luhaydaan. Wanachuoni wa al-Madiynah kama Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy, Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy, Shaykh ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy, Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy, Shaykh ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad na mwana wake Shaykh ´Abdur-Razzaaq, Shaykh Muhammad bin Rabiy´ al-Madkhaliy na wanachuoni wengine wa Salafiyyuun. Vivyo hivyo vitabu vya Shaykh Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy na mfano wavyo. Vyote hivi ni katika vitabu vyenye faida na vilivyo na manufaa. Vitabu vya Salafiyyuun katika kila zama na mahala ni vitabu vilivyo na manufaa na vizuri. Kunakhofiwa juu ya baadhi ya wanafunzi vitabu vya Hizbiyyuun.
- Muhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
- Imechapishwa: 23/07/2017
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)