Swali 25: Ni ipi hukumu ya mfungaji kufanya enema kwa sababu ya haja?

Jibu: Hukumu yake ni kwamba hakuna neno kufanya hivo iwapo mgonjwa atahitajia kufanya hivo kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Hilo ndio chaguo la Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) na wanachuoni wengi ambao wanaonelea kuwa kitendo hicho hakifanani na kula na kunywa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdllaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah tata´alaqah bisw-Swiyaam, uk. 29
  • Imechapishwa: 08/05/2019