23. Mwito kwa ajili ya swalah ya kupatwa kwa jua

Swali 23: Imepokelewa kwamba kunanadiwa katika swalah ya kupatwa kwa jua:

الصلاة جامعة

“Swalah ya pamoja.”

Je, yanasemwa mara moja au imesuniwa kuyakariri? Ni mara ngapi yanakaririwa?

Jibu: Imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha kunadiwe swalah ya kupatwa kwa jua kwa kusema:

الصلاة جامعة

“Swalah ya pamoja.”

Sunnah kwa mwenye kuita akariri hivo mpaka ayakinishe kuwa amewasikilizisha watu. Hilo halina kikomo maalum kutokana na tunavojua.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 18/08/2022