23. Mtu bora anayefuata baada ya Manabii na Mitume

´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa ni mkali inapokuja katika Uislamu. Hakusilimu isipokuwa katika mwaka wa tano baada ya utume. Ama kuhusu Abu Bakr aliingia katika Uislamu pale tu aliposikia ulinganizi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aliposikia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema ya kwamba ni Mtume wa Allaah alimwamini bila ya kusita. Allaah amuwie radhi.

Allaah aliupa nguvu Uislamu kwa ´Umar. Aliulinda Uislamu kupitia yeye. Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Hatukuacha kuwa na nguvu tangu aliposilimu ´Umar.” al-Bukhaariy (3864) na Fadhwaa-il-us-Swahaabah (368) ya Ahmad.

Walipambana kwa kiasi cha kwamba wakawa na fadhila nyingi kuwashinda wengine. Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) alindaa jeshi dhidi ya wenye kuritadi. Kisha akatuma jeshi kwenda ´Iraaq na Shaam kupambana kwa ajili ya Allaah. Allaah amuwie radhi!

Anafuatiwa na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye aliifungua miji, kueneza Uislamu na kusimamisha uadilifu juu ya ardhi. Aliijaza dunia kwa uadilifu. Alikuwa na fadhila nyingi. Allaah amuwie radhi! Moja katika fadhila zake (Radhiya Allaahu ´anh) ni kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Niliota kuwa nilipewa chombo kilicho na maziwa ndani yake. Nikanywa sana mpaka nikaona maziwa yanatoka kwenye makuja yangu. Kisha nikampa maziwa yaliyobaki ´Umar bin al-Khattwaab.” Wakasema: “Umefasiri hilo vipi, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Elimu.” al-Bukhaariy (3681) na Muslim (2391).

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema tena:

“Niliota ninawatazama watu waliokuwa wamevaa kanzu. Baadhi yao kanzu inawafika kwenye kifua na wengine ilikuwa ni chini ya hapo. Nilimwona pia ´Umar bin al-Khattwaab aliiburuta kanzu yake.” Wakasema: “Umefasiri hilo vipi, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Dini.” al-Bukhaariy (3691) na Muslim (2390).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 15/10/2016