Katika siku hii kuna mambo yanatakiwa kufanywa ambayo tunayapanga kama ifuatavyo:
1 – Kutoka kwenda katika uwanja wa ‘Iyd kwa sura nzuri. Kwa namna ya kwamba akiwa amejipamba kwa kilicho halali. Anafanya hivo kwa ajili ya kumwingiliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Asipuuze kujisafisha na kujipamba mpaka amchinje mnyama wake wa Udhhiyah, kama wafanyavyo baadhi ya watu. Aharakishe kwenda mapema ili apate kukaa karibu na imamu na kupata thawabu ya kungoja swalah.
2 – Ni Sunnah kuleta Takbiyr njiani anapoenda katika uwanj hadi imamu atoke kwa ajili ya swalah. Imamu anapoanza Khutbah, basi atakata Takbiyr. Isipokuwa kama imamu ataleta Takbiry basi naye ataleta Takbiyr pamoja naye.
3 – Ni Sunnah kupita njia tofauti. Kwa maana ya kwamba aende kwa njia moja na kurudi kwa njia nyingine, kwa mujibu wa riwaya kutoka kwa Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhuma):
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa siku ya ‘Iyd anapita njia tofauti.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy.
4 – Ni Sunnah katika ‘Iyd-ul-Adhhwaa kutokula chochote mpaka baada ya swalah. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya ´Abdullaah bin Buraydah kutoka kwa baba yake:
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa anatoka katika siku ya Fitwr mpaka ale, na hakuwa anakula katika siku ya Kuchinja mpaka aswali.”
Ameipokea at-Tirmidhiy.
5 – Swalah ya ‘Iyd ni Sunnah iliyosisitizwa na muislamu ajitahidi kuitekeleza. Aidha anapaswa kuhamasisha watoto wake kuihudhuria, hata watoto wadogo, kwa kuonesha nembo za ´ibaadah ya Kiislamu. Baadhi ya wanazuoni wameona kuwa ni wajibu.
6 – Baada ya swalah na Khutbah achinje mwenyewe ikiwa anajua kuchinja na ale kutoka katika nyama hiyo. Jengine ni kwamba awape zawadi jamaa na majirani na kuwapa nyama masikini. Inajuzu kuhifadhi nyama ya Udhhiyah. Ama katazo la kuhifadhi au kula nyama ya Udhhiyah baada ya siku tatu hilo limefutwa kwa mujibu wa maoni ya jopo kubwa la wanazuoni. Wengine wameona kuwa halijafutwa, bali iwapo watu wanahitaji basi kuhifadhi kunakatazwa. Haifai kuidharau nyama ya Udhhiyah au kutupa kitu chenye haja ya kusafishwa kwa kisingizio cha usumbufu wa kukisafisha. Bali miongoni mwa kushukuru ni kuitumia yote au kumpa mwingine anayehitaji, hata kama kutahitaji juhudi.
7 – Hakuna shida kupongezana kwa ajili ya ‘Iyd. Aidha inapasa kuwatembelea wazazi na jamaa. Kuwatembelea jamaa ni bora kuliko ndugu wa Kiislamu wa kawaida, kwa sababu muislamu ana wajibu kuanza na wale waliobeba haki kubwa zaidi na wenye uhusiano wa karibu zaidi wa undugu wa damu.
[1] Swahiyh-ul-Bukhaariy (1894) na tazama ”Fath-ul-Baariy” (4/243).
- Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 37-38
- Imechapishwa: 14/05/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 37-38
Imechapishwa: 14/05/2025
https://firqatunnajia.com/23-mambo-ya-kufanya-katika-siku-ya-iyd/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket