‘Abdullaah bin Qurṭw (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika siku iliyo kubwa zaidi mbele ya Allaah (Ta´ala) ni siku ya Kuchinja kisha ni siku ya Istaraahi.”[1]
Ameipokea Abu Daawuud kwa cheni ya wapokezi nzuri.
Hadiyth hii ni dalili ya fadhilah ya siku ya Kuchinja na kwamba ndiyo siku kuu zaidi mbele ya Allaah, nayo ni siku Kuu ya hijjah, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
Siku ya hijjah Kubwa ni siku ya Kuchinja.”
Ameipokea Abu Daawuud kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
‘Uqbah bin ‘Aamir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Siku ya ‘Arafah, siku ya Kuchinj na masiku ya Tashriyq ndizo sikukuu yetu sisi waislamu…”[2]
Wameipokea watunzi wa Sunan, isipokuwa Ibn Maajah, kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
‘Iyd ya Kuchinja ni bora kuliko ‘Iyd ya Fitwr, kwa sababu katika ‘Iyd ya kuchinja kuna kuswali na kuchinja. ´Iyd ya Fitwr ndani yake kuna kutoa swadaqah na kuswali. Kuchinja ni bora kuliko kutoa swadaqah. Isitoshe ni kwamba siku ya Kuchinja inakusanya utukufu wa mahali na wakati kwa ajili ya walio kwenye ´ibaadah ya hijjah.
[1] Muslim (1141).
[2] Ahmad (4/152), Abu Daawuud (2419), at-Tirmidhiy (773), an-Nasaa’iy (5/252) na wengineo. at-Tirmidhiy amesema:
”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh”.
Ni Swahiyh pia kwa mujibu wa Ibn Khuzaymah (2100) na Ibn Hibbaan (8/368).
- Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 36-37
- Imechapishwa: 14/05/2025
‘Abdullaah bin Qurṭw (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika siku iliyo kubwa zaidi mbele ya Allaah (Ta´ala) ni siku ya Kuchinja kisha ni siku ya Istaraahi.”[1]
Ameipokea Abu Daawuud kwa cheni ya wapokezi nzuri.
Hadiyth hii ni dalili ya fadhilah ya siku ya Kuchinja na kwamba ndiyo siku kuu zaidi mbele ya Allaah, nayo ni siku Kuu ya hijjah, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
Siku ya hijjah Kubwa ni siku ya Kuchinja.”
Ameipokea Abu Daawuud kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
‘Uqbah bin ‘Aamir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Siku ya ‘Arafah, siku ya Kuchinj na masiku ya Tashriyq ndizo sikukuu yetu sisi waislamu…”[2]
Wameipokea watunzi wa Sunan, isipokuwa Ibn Maajah, kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
‘Iyd ya Kuchinja ni bora kuliko ‘Iyd ya Fitwr, kwa sababu katika ‘Iyd ya kuchinja kuna kuswali na kuchinja. ´Iyd ya Fitwr ndani yake kuna kutoa swadaqah na kuswali. Kuchinja ni bora kuliko kutoa swadaqah. Isitoshe ni kwamba siku ya Kuchinja inakusanya utukufu wa mahali na wakati kwa ajili ya walio kwenye ´ibaadah ya hijjah.
[1] Muslim (1141).
[2] Ahmad (4/152), Abu Daawuud (2419), at-Tirmidhiy (773), an-Nasaa’iy (5/252) na wengineo. at-Tirmidhiy amesema:
”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh”.
Ni Swahiyh pia kwa mujibu wa Ibn Khuzaymah (2100) na Ibn Hibbaan (8/368).
Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 36-37
Imechapishwa: 14/05/2025
https://firqatunnajia.com/22-hadiyth-hakika-siku-iliyo-kubwa-zaidi-mbele-ya-allaah/