Miongoni mwa mambo yanayofanana na haya kwa baadhi ya sura ni yale yanayotajwa na wafasiri wengi wa Qur-aan katika mfano wa maneno Yake (Ta´ala):
الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ
”… wenye wafanyao subira, wanaosema ukweli, watiifu, watoaji mali katika Njia ya Allaah na waombao msamaha kabla ya alfajiri.”[1]
Wanasema kwamba wenye kusubiri ni Mtume wa Allaah (Swalla Allahu Alayhi Wasallam), wasemao ukweli ni Abu Bakr, watiifu ni ´Umar, wanaotoa katika njia ya Aallah ni ´Uthmaan na waombao msamaha ni ´Aliy. Wanasema kwamba:
مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ
”Muhammad ni Mtume wa Allaah na wale walio pamoja naye… ”
inamkusudia Abu Bakr,
أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ
”… ni wakali kwa makafiri… ”
inamkusudia ´Umar,
رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ
”… wanahurumiana baina yao.”
inamkusudia ´Uthmaan na:
تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا
“Utawaona wakirukuu na wakisujudu… ”[2]
inamkusudia ´Aliy. Ajabu zaidi kuliko hivo ni kwamba baadhi yao wanasema:
وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ
”Naapa kwa tini na zaytuni… ”[3]
inamkusudia Abu Bakr na ´Umar,
وَطُورِ سِينِينَ
”Naapa kwa mlima wa sinai.”
Inamkusudia ´Uthmaan na:
وَهَـٰذَا الْبَلَدِ الْأَمِينِ
”… naapa kwa mji huu wa amani!”[4]
Inamkusudia ´Aliy.
Mambo ya kikhurafi kama haya wakati mwingine yanafasiri tamko kwa njia ambayo haikufahamishwa kabisa na tamko. Hakuna chochote katika matamshi haya kinachowalenga kabisa watu hawa. Maneno Yake (Ta´ala):
وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا
“Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu… ”[5]
yote ni sifa zinazorejelea kundi moja la watu. Ndio kile kinachokusudiwa na wanasarufi wanapozungumza kuhusu mfuatano wa vihusishi. Kinachokusudiwa hapa ni kwamba zote hizi ni zinazotumika juu ya kitu kimoja – ni wale wote walio pamoja naye. Haiwezekani kabisa zote zinamzungumzisha mtu mmoja.
Wakati mwingine hufanya tamko lililoachiwa na lenye kuenea kufupika kwa mtu mmoja. Wanasema kwamba:
إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ
”Hakika si vyenginevyo mlinzi wenu ni Allaah na Mtume Wake na wale walioamini ambao wanasimamisha swalah na wanatoa zakaah hali ya kuwa wananyenyekea.”[6]
kwamba inamkusudia ´Aliy. Baadhi ya wengine husema:
وَالَّذِي جَاءَ بِالصِّدْقِ وَصَدَّقَ بِهِ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ
”Na yule aliyekuja na ukweli na akausadikisha – basi hao ndio wenye uchaji.”[7]
kwamba inamkusudia Abu Bakr peke yake. Wengine husema:
لَا يَسْتَوِي مِنكُم مَّنْ أَنفَقَ مِن قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِّنَ الَّذِينَ أَنفَقُوا مِن بَعْدُ وَقَاتَلُوا
“Halingani sawa miongoni mwenu aliyejitolea kabla ya u shindi [wa ufunguzi wa mi wa Makkah] na akapigana, hao watapata daraja kuu kabisa kuliko wale waliotoa baadae na wakapigana… ”[8]
kwamba inamkusudia Abu Bakr peke yake.
[1] 03:17
[2] 48:29
[3] 95:1
[4] 95:2
[5] 48:29
[6] 5:55
[7] 39:33
[8] 57:10
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 78-80
- Imechapishwa: 07/04/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)