23. Je, mwenye kujiua anaoshwa na kuswaliwa?

Swali 23: Je, mwenye kujiua anaoshwa na kuswaliwa[1]?

Jibu: Anayejiua nafsi yake anaoshwa, anaswaliwa na anazikwa pamoja na waislamu. Kwa sababu ni mtenda dhambi na sio kafiri. Kujiua ni maasi na sio ukafiri. Akiua nafsi yake – najilinda kwa Allaah – basi anaoshwa, anavikwa sanda na kuswaliwa. Lakini kiongozi mkuu na wale watu muhimu wanatakiwa kuacha kumswalia kwa minajili ya makemeo. Lengo ni ili watu wasije kudhani kuwa wameridhia kitendo chake. Kiongozi mkuu, mfalme, mahakimu, raisi au kiongozi wa nchi ni vizuri wakiacha kufanya hivo kwa lengo la kukemea jambo hilo na kutangaza kuwa kitendo hicho ni makosa. Lakini wamswalie baadhi ya waswaliji.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/123).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 17/12/2021