24. Vipi anaoshwa aliyekufa katika ajali na mwili wake umekatikakatika?

Swali 24: Vipi anaoshwa mtu ambaye anakufa katika ajali na mwili wake unaharibika na pengine vikakatika baadhi ya viungo vyake? Tunamwomba Allaah usalama na afya[1].

Jibu: Ni lazima kumwosha kama wanavooshwa wengine, ikiwezekana kufanya hivo. Isipowezekana basi atafanyiwa Tayammum. Kwa sababu Tayammum inasimama mahali pa kuosha kwa maji wakati inaposhindikana kufanya hivo.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/123).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 23
  • Imechapishwa: 17/12/2021