Asijifunze isipokuwa kwa yule aliyekamilika uwezo wake, dini yake imeonekana, maarifa yake yamethibiti na uadilifu wake umejulikana. Muhammad bin Siyriyn, Maalik bin Anas na wengineo miongoni mwa Salaf amesema:
”Elimu hii ni dini. Hivyo basi kuweni waangalifu mnachukua dini yenu kutoka kwa nani.”
Aidha anatakiwa amwangalie mwalimu wake kwa jicho la heshima. Aamini ukamilifu wa uwezo wake na ubora wake juu ya watu wa daraja lake. Kwani hilo ni karibu zaidi na kunufaika kwake naye. Baadhi ya waliotangulia walikuwa wanapokwenda kwa mwalimu wao wanatoa swadaqah kwa kitu fulani na wanasema:
”Ee Allaah! Nifiche kasoro za mwalimu wangu kwangu na wala usiniondolee baraka ya elimu yake.”
ar-Rabiy´, swahiba wa ash-Shaafi´iy (Rahimahumaa Allaah), amesema:
”Sikuthubutu kunywa maji huku ash-Shaafi´iy ananitazama kwa sababu ya kumheshimu.”
Tumesimuliwa kwamba Kiongozi wa waumini ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Miongoni mwa haki za mwalimu juu yako ni kwamba uwape watu wote salamu kwa ujumla na umtenganishe yeye kwa salamu maalum, ukae mbele yake, usiashirie mkono wako mbele yake, usipepese macho yako, usimtajie maoni tofauti ya mwengine, usimsengenye mtu yeyote mbele yake, usishauriane na mwenzako katika kikao chake, usimshike vazi lake anaposimama, usimsumbue anapochoka na wala usichoke kwa muda mrefu wa kukaa naye.”
Inampasa ajipambe na sifa hizi alizoelekeza ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Isitoshe ajibu usengenyi anaofanyiwa mwalimu wake akiweza kufanya hivo. Ikiwa hawezi kuzuia, basi aondoke katika kikao hicho.
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 34
- Imechapishwa: 26/08/2026
Asijifunze isipokuwa kwa yule aliyekamilika uwezo wake, dini yake imeonekana, maarifa yake yamethibiti na uadilifu wake umejulikana. Muhammad bin Siyriyn, Maalik bin Anas na wengineo miongoni mwa Salaf amesema:
”Elimu hii ni dini. Hivyo basi kuweni waangalifu mnachukua dini yenu kutoka kwa nani.”
Aidha anatakiwa amwangalie mwalimu wake kwa jicho la heshima. Aamini ukamilifu wa uwezo wake na ubora wake juu ya watu wa daraja lake. Kwani hilo ni karibu zaidi na kunufaika kwake naye. Baadhi ya waliotangulia walikuwa wanapokwenda kwa mwalimu wao wanatoa swadaqah kwa kitu fulani na wanasema:
”Ee Allaah! Nifiche kasoro za mwalimu wangu kwangu na wala usiniondolee baraka ya elimu yake.”
ar-Rabiy´, swahiba wa ash-Shaafi´iy (Rahimahumaa Allaah), amesema:
”Sikuthubutu kunywa maji huku ash-Shaafi´iy ananitazama kwa sababu ya kumheshimu.”
Tumesimuliwa kwamba Kiongozi wa waumini ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Miongoni mwa haki za mwalimu juu yako ni kwamba uwape watu wote salamu kwa ujumla na umtenganishe yeye kwa salamu maalum, ukae mbele yake, usiashirie mkono wako mbele yake, usipepese macho yako, usimtajie maoni tofauti ya mwengine, usimsengenye mtu yeyote mbele yake, usishauriane na mwenzako katika kikao chake, usimshike vazi lake anaposimama, usimsumbue anapochoka na wala usichoke kwa muda mrefu wa kukaa naye.”
Inampasa ajipambe na sifa hizi alizoelekeza ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Isitoshe ajibu usengenyi anaofanyiwa mwalimu wake akiweza kufanya hivo. Ikiwa hawezi kuzuia, basi aondoke katika kikao hicho.
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 34
Imechapishwa: 26/08/2026
https://firqatunnajia.com/23-heshima-kwa-mwalimu/