Yote tuliyoyataja miongoni mwa adabu za mwalimu katika nafsi yake ni adabu pia kwa mwanafunzi. Miongoni mwa adabu zake ni kwamba ajiepushe na sababu zinazomshughulisha na kumzuia kupata elimu isipokuwa sababu isiyoweza kuepukika kwa haja. Aidha inampasa ausafishe moyo wake kutokana na uchafu ili uwe mzuri kwa kuipokea Qur-aan, kuihifadhi na kunufaika nayo. Kwani imesihi ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika katika mwili kuna kipande cha nyama; kikitengenea mwili wote hutengenea, na kikiharibika mwili wote huharibika. Nacho ni moyo.”
Amesema vyema msemaji kwa kusema:
”Moyo hutengenea kwa ajili ya elimu kama ardhi inavyotengenea kwa ajili ya kilimo.”[1]
Inampasa anyenyekee kwa mwalimu wake na awe na adabu pamoja naye hata kama ni mdogo kwake kwa umri, mdogo kwa umaarufu, nasaba au wema. Anatakiwa ainyenyekee elimu, kwa sababu kwa unyenyekevu wake ataipata. Walikuwa wakisema:
Elimu ni vita kwa kijana mwenye kiburi
kama ilivyo kwa mafuriko ni vita kwa sehemu iliyo juu
Inampasa ajisalimishe kwa mwalimu wake, amshauri katika mambo yake na akubali maneno yake kama mgonjwa mwenye akili anavyokubali maneno ya tabibu mnasihi na mwenye ujuzi. Hili la kwanza ni lenye kufaa zaidi.
[1] al-Bukhaariy (52) na Muslim (1599).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 33-34
- Imechapishwa: 26/08/2026
Yote tuliyoyataja miongoni mwa adabu za mwalimu katika nafsi yake ni adabu pia kwa mwanafunzi. Miongoni mwa adabu zake ni kwamba ajiepushe na sababu zinazomshughulisha na kumzuia kupata elimu isipokuwa sababu isiyoweza kuepukika kwa haja. Aidha inampasa ausafishe moyo wake kutokana na uchafu ili uwe mzuri kwa kuipokea Qur-aan, kuihifadhi na kunufaika nayo. Kwani imesihi ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika katika mwili kuna kipande cha nyama; kikitengenea mwili wote hutengenea, na kikiharibika mwili wote huharibika. Nacho ni moyo.”
Amesema vyema msemaji kwa kusema:
”Moyo hutengenea kwa ajili ya elimu kama ardhi inavyotengenea kwa ajili ya kilimo.”[1]
Inampasa anyenyekee kwa mwalimu wake na awe na adabu pamoja naye hata kama ni mdogo kwake kwa umri, mdogo kwa umaarufu, nasaba au wema. Anatakiwa ainyenyekee elimu, kwa sababu kwa unyenyekevu wake ataipata. Walikuwa wakisema:
Elimu ni vita kwa kijana mwenye kiburi
kama ilivyo kwa mafuriko ni vita kwa sehemu iliyo juu
Inampasa ajisalimishe kwa mwalimu wake, amshauri katika mambo yake na akubali maneno yake kama mgonjwa mwenye akili anavyokubali maneno ya tabibu mnasihi na mwenye ujuzi. Hili la kwanza ni lenye kufaa zaidi.
[1] al-Bukhaariy (52) na Muslim (1599).
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 33-34
Imechapishwa: 26/08/2026
https://firqatunnajia.com/22-yanayopasa-kupatilizwa-na-mwanafunzi/