Hadiyth ya nane

وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ

“Na utabakia uso wa Mola Wako wenye utukufu na wenye ukarimu.”[1]

100 – Abu ´Abdillaah Muhammad bin ´Aliy bin Wahb amenihadithia kwa kunisomea Kairo: Nilimsomea Abul-Hasan ash-Shaafi´iy: Abut-Twaahir as-Silafiy ametuhadithia: Abu ´Abdillaah ath-Thaqafiy ametuhadithia: ´Aliy bin Muhammad ametuhadithia: Ismaa´iyl as-Swaffaar ametuhadithia: Sa´daan ametuhadithia: Ibn ´Uyaynah ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr ambaye ameeleza kuwa amemsikia Jaabir akisema:

”Wakati Aayah:

قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَىٰ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ

“Sema: “Yeye ni muweza wa kukutumieni adhabu kutoka juu yenu… ”

ilipoteremshwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), alisema:

”Najilinda na uso Wako.”

na:

أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ

”… au kutoka chini ya miguu yenu… ”

akasema:

”Najilinda na uso Wako.”

na:

أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعًا وَيُذِيقَ بَعْضَكُم بَأْسَ بَعْضٍ

”… au akutatanisheni mfarikiane kuwa makundimakundi na akuonjesheni baadhi yenu nguvu za wengineo.”[2]

Akasema: ”Afadhali haya mawili au ni mepesi.”[3]

Hadiyth ni Swahiyh.

101 – Miongoni mwa maudhui hayo ni kwamba Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituhutubia mambo matano na kusema: “Allaah halali na wala haimstahikii Yeye kulala. Anaishusha mizani na kuinyanyua. Kwake kunapandishwa matendo ya usiku kabla ya mchana na matendo ya mchana kabla ya usiku. Pazia Yake ni Nuru; lau ataifunua, basi mwanga wa uso Wake ungeliunguza kila anachoona katika uumbaji Wake.”[4]

102 –  Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema tena:

”Hakika Mola wenu hana usiku wala mchana. Nuru ya mbingu na ardhi inatokana na nuru ya uso Wake.”

103 – Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

اللهم إني أَسْأَلكَ لَذَّةَ النَّظرِ إِلى وَجْهِكَ وَالشَّوْقَ إِلَى لِقَائِكَ

”Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba ladha ya kutazama uso Wako na kutamani kukutana Nawe.”[5]

104 – Ibn Mas´uud amesema:

”Mwenye kusema:

سبحان الله و الحمد لله و الله اكبر

”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu, himdi zote njema anastahiki Allaah na Allaah ni mkubwa.”,

anayapokea Malaika na kumpelekea nayo Allaah (Ta´ala). Hapiti kundi lolote la Malaika isipokuwa wanamuombea msamaha aliyeyatamka mpaka wafike nayo kwenye uso wa Allaah.”

105 – Abu Bakr as-Swiddiyq, Hudhayfah, Abu Muusa na Maswahabah wengine (Radhiya Allaahu ´anhum) wamesema kuhusu maneno Yake Allaah (Ta´ala):

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ

“Kwa wale waliofanya mazuri watapata Pepo na zaidi.”[6]

”Watatazama uso wa Allaah (Ta´ala).”[7]

Allaah (Ta´ala) amesema:

وكُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

“Kila kitu ni chenye kuangamia isipokuwa uso Wake.”[8]

[1]55:27

[2] 6:65

[3] Muslim (179).

[4] Muslim (179).

[5] an-Nasaa’iy (1305) na ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan (509 – al-Mawaarid) na al-Albaaniy katika ”as-Sunnah” (424).

[6] 10:26

[7] Jaamiy´-ul-Bayaan (12/155-165).

[8] 28:88

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 105-109
  • Imechapishwa: 09/06/2024