Miongoni mwa waliosema kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi kwa dhati Yake ni Imaam Yahyaa bin ´Ammaar na Imaam Abu Naswr as-Sijziy, ambaye amesema katika kitabu “al-Ibaanah”:

“Maimamu wetu kama ath-Thawriy, Maalik, Ibn ´Uyaynah, Hammaad bin Salamah, Hammaad bin Zayd, Ibn-ul-Mubaarak, al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw, Ahmad na Ishaaq, wameafikiana ya kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi kwa dhati Yake na kwamba ujuzi Wake uko kila sehemu.”

Hivyo hivyo kasema Shaykh-ul-Islaam al-Answariy:

“Kuna mapokezi mengi yanayosema kuwa Allaah yuko juu ya mbingu ya saba juu ya ´Arshi.”

Hivyo pia ndivo kasema rafiki yake Abul-Hasan al-Karajiy katika utenzi wake kuhusu ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah:

´Aqiydah yao ni kwamba Mola kwa dhati Yake

yuko juu ya ´Arshi, pamoja na utambuzi Wake wa mambo ya ghaibu

Imaam Abul-Qaasim al-Laalakaa’iy ash-Shaafi´iy amesema:

“Mapokezi cha yale yaliyopokelewa kuhusiana na maneno Yake  (Ta´ala):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

na kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake juu ya mbingu.

Amesema (´Azza wa Jall):

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake linapanda neno zuri na tendo zuri hulitukuza.”[2]

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ

“Je, mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokudidimizeni ardhini?”[3]

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ

“Naye  ni Mwenye kutenza nguvu juu ya waja Wake.”[4]

Aayah hizi zinathibitisha ya kwamba Yeye  (´Azza wa Jall) yuko juu mbinguni na kwamba utambuzi Wake umezunguka kila maeneo.

Haya yamesimuliwa kutoka kwa Maswahabah wafuatao:

”´Umar, Ibn Mas´uud, Ibn ´Abbaas na Umm Salamah.”

Haya yamesimuliwa kutoka kwa wanafunzi wa Maswahabah wafuatao:

Rabiy´ah bin Abiy ´Abdir-Rahmaan, Sulaymaan at-Taymiy na Muqaatil bin Hayyaan.

Yamesemwa na wanazuoni kama:

Maalik bin Anas, Sufyaan ath-Thawriy na Ahmad bin Hanbal.”[5]

[1] 20:5

[2] 35:10

[3] 67:16

[4] 6:61

[5] Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah (3/387-402).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 78-80
  • Imechapishwa: 29/12/2025