Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah (Ta´ala) amesema:

فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا ۚ فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚلَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

“Basi elekeza uso wako katika dini yenye imani safi na iliyotakasika, imani hiyo ndio maumbile Allaah aliyowaumbia watu [wote] – hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Allaah! Hivyo ndio dini iliyonyooka sawasawa, lakini watu wengi hawajui. (30:30)

وَوَصَّىٰ بِهَا إِبْرَاهِيمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَا بَنِيَّ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ لَكُمُ الدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ

 “Na Ibraahiym akawausia hayo wanawe na [kadhalika] Ya’quub [akawaambia]: “Enyi wanangu! Hakika Allaah amekuchagulieni nyinyi dini; hivyo basi msife isipokuwa nyinyi ni waislamu.” (02:132)

ثُمَّ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ أَنِ اتَّبِعْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ

 “Kisha Tukakufunulia Wahy kwamba fuata imani ya Ibraahim iliyo safi na kutakasika na hakuwa miongoni mwa washirikina.” (16:123)

Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kila Mtume ana msaidizi katika Mitume na mimi msaidizi wangu katika wao ni baba yangu na Khaliyl wa Allaah Ibraahiym.” Halafu akasoma:

إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَـٰذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا ۗوَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ

“Hakika watu waliokaribu zaidi kwa Ibraahiym ni wale waliomfuata, kama mfano wa Nabii huyu na wale walioamini. Na Allaah ni Mlinzi wa waumini.”[1] (03:68)

Ameipokea at-Tirmidhiy.

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Uislamu ulianza ni kitu kigeni na utarudi kuwa kitu kigeni kama ulivyoanza. Hivyo Twubaa kwa wale wageni!”

Ameipokea Muslim.

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah hatazami miili yenu wala mali zenu; anatazama nyoyo zenu na matendo yenu.”[2]

MAELEZO

Allaah hatazami miili yenu… – Hii ni Hadiyth Swahiyh ameitoa Muslim:

“Allaah hatazami miili yenu wala mali zenu; anatazama nyoyo zenu na matendo yenu.”

Nyoyo ndio sehemu inayotazamwa na matendo. Kuhusu sura na mali haina maana yoyote isipokuwa ikiwa kama itatumika katika kumtii Allaah. Lakini kinachotazamwa ni nyoyo ikiwa zitanyooka juu ya kumpenda Allaah, kumtakasia nia, kumwogopa, kumtarajia, matendo yakatengenezwa na yakawa yamefanywa kwa ajili ya Allaah pekee na wakati huohuo yameafikiana na Sunnah, haya ndio mambo yanayomfaa mwenye nayo. Inahusiana na kutengemaa kwa moyo na matendo.

[1] at-Tirmidhiy (2995), al-Bazzaar (5/345) na al-Haakim (2/320).

[2] Muslim (2564).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 04/11/2020