22. ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz akihimiza Sunnah na akitahadharisha Bid´ah

2 – Miongoni mwa maneno ya wanafunzi wa Maswahabah amesema kiongozi wa waumini ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz ambaye amezaliwa mwaka wa 63 na amekufa mwaka wa 101. Maneno yake yamebeba ujumbe ufuatao:

1 – Ulazima wa kusimama pale waliposimama watu akiwa na maana ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake katika ile dini waliyokuwemo kiimani na kimatendo. Kwa sababu walisimama kwa ujuzi na utambuzi. Endapo kungelikuwa kuna kheri katika yale yaliyozuliwa na wa baada yao basi wangelikuwa na haki zaidi.

2 – Yaliyozuliwa baada yao hakuna jingine ndani yake isipokuwa kwenda kinyume na uongofu wao na kuipa mgongo Sunnah yao. Vinginevyo wameeleza kuhusu dini yanayokidhi na wamezungumza juu yake yanatosheleza.

3 – Baadhi yao wamefanya upungufu katika kuwafuata na wakawa wenye kuzembea na wengine wakavuka mipaka waliyokuwemo wakawa wenye kupetuka mpaka. Njia ilionyooka ni ile iliyo kati ya kuchupa mpaka na kuzembea.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 43
  • Imechapishwa: 14/10/2022