22. Sababu ya kumi na nane ya talaka ambayo ni mwanamke kutoka nyumbani saa zote

18 – Mwanamke aliye mbali na nyumba yake

Kuna mwanamke ambaye yeye siku zote yuko mbali. Mwanamke ikawa siku zote yeye anatoka kwenda kazini na mwanamke huyo akaona kuwa maisha yamebadilika. Huu ndio uhalisia wetu, enyi ndugu zangu. Mimi nazungumzia uhalisia wa hali. Imekuwa mwanamke anatamani kushiriki katika kazi kwa kumuigiliza mwanaume. Hii ndio vita waliyotupiga watu wa mashariki na watu wa magharibi na usawa baina ya mwanaume na mwanamke. Baadhi ya wanawake wakang´ang´ania kipengele hichi na wakaghurika nacho. Mosi ni kwamba baadhi ya wanaume hawapendezwi na jambo hili. Pili ni kwamba wanahisi hawana haja ya msaada huo. Aidha wanaona kuwa mwanamke huyu kutilia umuhimu nyumba yake, watoto wake na yeye mwenyewe ndio muhimu zaidi kuliko kazi hiyo, jambo ambalo ndio la sawa. Mume anataka wakati anapoenda nyumbani amkute mke wake mbele yake. Hataki kumuona yule dada wa kazi. Wakati mwingine mume akitaka kitu kutoka kwa mke wake anamjibu kwamba amechoka na kazi na kwamba yeye amechoka kama yeye.

Tukikadiria kuwa kazi hiyo imepatikana kwa maafikiano yao, kwa msemo mwingine mume amemruhusu yeye kufanya kazi, basi ni lazima kwa mke kukusanya kati ya kazi na kumtekelezea haki mume, watoto wake na nyumba yake.  Asiwanyime haki zao kwa sababu eti ya kazi. Huenda mwanamke huyo akakosa kwa mume wake zile hisia za ukaribu wake yule mume, kushirikiana naye katika nyanja zake zote za maisha na umuhimu wake, jambo ambalo hupelekea kukatokea magomvi kati yao na pengine ikafikia katika talaka.

Wakati mwingine inatokea yule mume anakuwa katika shughuli inayomshughulisha na nyumba na watoto wake kwa sababu ya kushughulishwa kwake mwanamke na kutilia umuhimu wenye kuzidi kujipamba, kwenda kwa msukaji, maduka ya nguo na masaluni ya kujipamba na hivyo akaipuuza nyumba. Mimi najua familia fulani, bali ukoo, walijishughulisha kwenda na kurudi katika maduka ya nguo, maduka ya mapambo na kutunza uzuri wa mwili. Hali ilifikia kwenda katika zile sehemu za kukandwa. Yote hayo kwa ajili ya kutunza uzuri wa mwili wake na kutilia umuhimu wa kupindukia juu ya nafsi yake na akampuuza mume na watoto wake. Ni kipi anachovuna mume huyu kutoka kwa mke huyu na yeye ni mwenye kuingia na mwenye kutoka. Hayo hatimaye yanapelekea kumalizika subira ya mwanaume huyu na hivyo ikapelekea katika talaka.

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 36-38
  • Imechapishwa: 18/04/2024