22. Masimulizi ya Maalik kwa mujibu wa wasimulizi kutoka kwa maswahiba wa Maalik

10 – Upokezi wa Sahnuun[1] kutoka kwa maswahiba zake Maalik

Ibn Rushd amesema:

“Sahnuun akasema: “Mmoja wa marafiki zake Maalik amenikhabarisha kwamba alikuwa kwa Maalik wakati mtu mmoja alipomjia na kusema: “Ee Abu ´Abdillaah, nina swali.” Akakaa kimya. Akasema kwa mara nyingine: “Ee Abu ´Abdillaah, nina swali.” Akaendelea kukaa kimya. Akauliza kwa mara ya tatu, ambapo Maalik akainua kichwa kwa lengo la kumjibu. Akasema: “Ee Abu ´Abdillaah!

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[2]

Ilikuweje kulingana Kwake juu?” Maalik akainamisha kichwa chake kwa muda kisha akakiinua na kusema: ”Umeuliza juu ya kitu ambacho si kwamba hakitambuliki na umezungumzia kisichofahamika. Sikuoni vyengine isipokuwa mtu muovu. Mtoeni nje!”[3]

[1] Imaam, ´Allaamah na mwanachuoni wa Afrika Kaskazini, Abu Sa’iyd ´Abdus-Salaam bin Habiyb bin Hassaan at-Tannuukhiy. Jaji wa Qayrawaan na mtunzi wa “al-Mudawwanah”.

Amesikia kutoka kwa Sufyaan bin ´Uyaynah na akalazimiana na wanafunzi wa Maalik Ibn Wahb, Ibn-ul-Qaasim na Ash-hab mpaka akawa analingana nao. Alikufa mwaka 240. Tazama “Siyar A´laam-in-Nubalaa’” (12/63-69).

[2] 20:05

[3] al-Bayaan wat-Tahswiyl (16/367-369).

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 41
  • Imechapishwa: 30/11/2025