22. Je, al-Albaaniy ana wafuasi Saudi Arabia?

Je, al-Albaaniy ana wafuasi Saudi Arabia? Mimi sijui kama ana wafuasi nchini kwa sababu sitambui kuwa ana ´Aqiydah ya kipekee wala Salafiyyah ya kipekee mpaka awe na wafuasi.

Je, anaonelea kwamba ni lazima kula kiapo cha usikivu na utiifu juu ya mamlaka ya Saudi Arabia? Ndio, kwa vile anaiita Saudi Arabia “Nchi ya Tawhiyd” na yeye, kama walivyo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na Salafiyyuun wengine wote, hajuzishi kumfanyia uasi mtawala wa waislamu. Hayo yanathibitishwa kupitia taaliki yake juu ya “Sharh at-Twahaawiyyah” ya Ibn Abiyl-´Izz al-Hanafiy ambapo amesema waziwazi kwamba ni wajibu kushikamana na mkusanyiko na kumtii mtawala na kwamba haifai kufanya uasi dhidi yake.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 44
  • Imechapishwa: 03/12/2018