Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ
”Na fanyeni wema – hakika Allaah anapenda watendao wema.” (02:195)
وَأَقْسِطُوا ۖ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِين
”… na fanyeni haki. Hakika Allaah anapenda wafanyao haki.” (49:09)
فَمَا اسْتَقَامُوا لَكُمْ فَاسْتَقِيمُوا لَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ
”Basi wakikunyokeeni [kwa uzuri], nanyi wanyokoeeni [kwa uzuri]. Hakika Allaah anapenda wamchao.” (09:07)
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ
”Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni atakupendeni Allaah.” (03:31)
فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ
”Basi Allaah ataleta watu [badala yao] atakaowapenda nao watampenda.” (05:54)
إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفًّا كَأَنَّهُم بُنْيَانٌ مَّرْصُوصٌ
”Hakika Allaah anapenda wale wanaopigana katika njia Yake safu kwa safu kama kwamba wao ni jengo linalokamatana barabara.” (61:04)
وَهُوَ الْغَفُورُ الْوَدُودُ
“Naye ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye mapenzi halisi.” (85:14)
MAELEZO
Aayah hizi nyingi ndani yake mna sifa ya kupenda. Allaah amejieleza Mwenyewe kwa sifa ya kupenda, kwamba anapenda na kupendwa na kwamba anawapenda wachaji Allaah, watendao wema na kwamba anawapenda wafanyao uadilifu. Amesema (Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهٍُ
”Enyi mlioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka dini yake, basi Allaah atawaleta watu [badala yao] atakaowapenda nao watampenda.” (05:54)

”Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni, atakupendeni Allaah.” (03:31)
Vilevile Yeye ni Mwingi wa rehema na Mwenye kurehemu. Huruma Yake imeenea kwenye kila kitu. Yeye ni mwenye kusamehe na kwamba ni mwenye mapenzi halisi. Mapenzi halisi maana yake ni kwamba anapenda na kupendwa.
Ni mwenye kuridhia, hughadhibika, huchukia na hukirihika:
رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ
”Allaah ataridhika nao, nao wataridhika Naye.” (98:08)
غَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِم
“Allaah ameghadhibika nao.” (48:14)
اتَّبَعُوا مَا أَسْخَطَ اللَّـهَ وَكَرِهُوا رِضْوَانَهُ
“… wamefuata yale yanayomghadhibisha Allaah na wakachukia radhi Zake.” (47:28)
وَلَـٰكِن كَرِهَ اللَّـهُ انبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ
”Lakini Allaah Amechukia kutoka kwao, basi Akawazuia.” (09:46)
Zote hizi ni sifa za haki. Radhi, mapenzi, rehema, kukasirika na kuchukia. Zote hizi anasifiwa nazo (Jalla wa ´Alaa). Ni kama sifa nyenginezo ambazo zinalingana na Allaah pekee. Mtu anatakiwa kuzithibitisha bila ya kupotosha, kukanusha, kuzifanyia namna na kuzipigia mfano. Kupenda Kwake sio kama wanavyopenda viumbe, kuridhia Kwake sio kama kuridhia kwa viumbe, kuchukia Kwake sio kama wanavyochukia viumbe. Vivyo hivyo inahusiana na sifa nyenginezo. Kanuni hiyohiyo ndio inayotumika juu ya sifa zingine zote. Amesema (Ta´ala):
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni kusikia, Mwenye kuona.” (42:11)
وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
“… na wala hana yeyote anayefanana [wala kulingana] Naye.” (112:04)
فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ
”Basi msipigie mifano Allaah!” (16:74)
Bi maana hana anayefanana Naye. Usimpigie Allaah mifano. Kwani Allaah hana mwenza na hana mshirika. Sifa zote zinatakiwa kufahamika namna hiyohiyo.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waaswitiyyah, uk. 31-32
- Imechapishwa: 21/10/2024

Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waaswitiyyah, uk. 31-32
Imechapishwa: 21/10/2024
https://firqatunnajia.com/22-dalili-ya-kupenda-na-kuchukia-kwa-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)