22. Asiyeswali atafufuliwa na makafiri

2- Atafufuliwa na makafiri na washirikina kwa sababu yeye ni katika wao. Allaah (Ta´ala) amesema:

احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ فَاهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْجَحِيمِ

“Wakusanyeni wale waliodhulumu na wenziwao na yale waliyokuwa wakiyaabudu badala ya Allaah, na waongozeni kwenye njia ya Motoni.”[1]

Wenziwao hapa kunakusudiwa watu sampuli yao, nao ni ´wale waliodhulumu na watu aina yao hao hao katika makafiri na wadhulumaji’.

[1] 37:22-23

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Hukm Taarik-is-Swalaah, uk. 22
  • Imechapishwa: 22/10/2016