21. Asiyeswali anapewa kipigo kizito wakati wa kufa

Hapa kunafuata baadhi ya hukumu za kuritadi zinazohusiana na Aakhirah:

1- Malaika wanamkemea na kumkataa na bali wanampiga uso na mgongo wake. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ يَتَوَفَّى الَّذِينَ كَفَرُوا ۙ الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيكُمْ وَأَنَّ اللَّـهَ لَيْسَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ

“Na lau ungeliona pale Malaika wanapowafisha wale waliokufuru wanawapiga nyuso zao na migongo yao [na huku wakiwaambia]: “Onjeni adhabu iunguzayo, hayo ni kwa yale yaliyotangulizwa na mikono yenu; na Allaah si Mwenye kuwadhulumu waja Wake.”[1]

[1] 08:50-51

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Hukm Taarik-is-Swalaah, uk. 22
  • Marejeo: Firqatunnajia.com
  • Imechapishwa: 22/10/2016