Swali 22: Je, anaoshwa mwenye kudhulumiwa[1]?

Jibu: Ndio, anaoshwa na kuswaliwa. ´Umar al-Faaruq (Radhiya Allaahu ´anh) aliuliwa hali ya kudhulumiwa. ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) aliulizwa hali ya kudhulumiwa. Licha ya hivo alioshwa na Maswahabah wakamswalia. Vivyo hivyo ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) aliuliwa hali ya kudhulumiwa ambapo akaoshwa na kuswaliwa.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/122).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 22
  • Imechapishwa: 16/12/2021