21. Kumuosha mjeruhi wa uwanja wa vita akifa baada ya hapo

Swali 21: Aliyekufa katika uwanja wa vita hali ya kuwa ni mwenye kuathirika kwa majeraha yake anaoshwa, anavikwa sanda na kuswaliwa?

Jibu: Ndio. Anaoshwa, anavikwa sanda na kuswaliwa. Kunatarajiwa juu yake ujira wa aliyekufa shahidi akitakasa nia yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 22
  • Imechapishwa: 16/12/2021