21. Ni ipi hukumu ya kukata swawm kwa adhaana inayotolewa dakika tano kabla ya jua kuzama?

Swali 21: Ni ipi hukumu ya kufungua swawm kwa adhaana inayoadhiniwa dakika tano kabla ya jua kuzama?

Jibu: Ikiwa wamefungua wakati jua bado laonekana basi ni wajibu kwao kulipa siku hiyo. Ama ikiwa jua halionekani kwa sababu ya mawingu au mfano wa hayo na mara nyingi kunaadhiniwa dakika tano kabla ambapo ima kitu katika jua kinaonekana au lote kabisa, lililo salama zaidi ni yeye kuilipa siku hiyo.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 12/06/2017