21. Kufurahi kwa kuelewa maana sahihi ya Shahaadah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1 – Faida ya kwanza: Ni kufurahi kwa fadhilah na rehema za Allaah. Kama Alivyosema Allaah (Ta´ala):

قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ

“Sema: “Kwa fadhilah za Allaah na kwa rehema Zake basi kwa hayo wafurahi.” Hayo ni kheri kuliko wanayoyakusanya.”” (10:58)

MAELEZO

Hili linapatikana kwa njia mbili:

1 – Allaah (Ta´ala) amekutunukia mpaka ukaweza kuelewa maana sahihi ya maneno haya makubwa “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah”. Hii ni fadhilah kubwa ya Allaah na rehema Zake. Allaah ameamrisha mtu kufurahi kwa neema kama hii. Dalili ya hili ni ile ambayo mtunzi (Rahimahu Allaah) ametaja:

قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ

“Sema: “Kwa fadhilah za Allaah na kwa rehema Zake basi kwa hayo wafurahi.” Hayo ni kheri kuliko wanayoyakusanya.”” (10:58)

Mja kufurahi kwa ajili ya elimu na ´ibaadah ambayo Allaah amemtunukia ni miongoni mwa mambo yenye kusifiwa. Imekuja katika Hadiyth:

“Mfungaji anazo furaha mbili; pindi anapofungua swawm na wakati atapokutana na Mola Wake.”[1]

[1] al-Bukhaariy (1904) na Muslim (165).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Fitqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 44
  • Imechapishwa: 23/04/2022