21. Mfano wa vichenguzi vya Uislamu

Hii ndio misingi sita ya imani iliyotajwa katika Hadiyth ya Jibriyl (´alayhis-Salaam). Kwa hivyo ni lazima kwa muumini kuihakikisha na kuiamini. Aidha ni lazima pia kutamka shahaadah mbili; kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Mtu afanye hivo kwa utambuzi, yakini, ukweli, mapenzi, kutakasa nia, kunyenyekea na kukubali. Ni lazima pia, baada ya kuamini, mtu atende vile zinavyopelekea shahaadah hizi mbili. Mtu ajiepushe na kichenguzi miongoni mwa vichenguzi vya imani na Tawhiyd na asipinge jambo linalotambulika vyema ndani ya Uislamu.

Miongoni mwa mifano ya vichenguzi vya imani na Tawhiyd ni shirki kubwa. Mfano wake mtu amfanyie aina moja wapo miongoni mwa aina za ´ibaadah kumfanyia asiyekuwa Allaah, amswalie, amfungie au amuhijie mwingine asiyekuwa Allaah, amuombe asiyekuwa Allaah, aombe msaada kutoka kwa asiyekuwa Allaah, amchinjie au amuwekee nadhiri mwingine asiyekuwa Allaah, atufu kwengine isiyokuwa Ka´bah hali ya kujikurubisha kwa asiyekuwa Allaah, amsujudie au kumfanyia Rukuu´ mwingine asiyekuwa Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 28
  • Imechapishwa: 02/05/2023