21. Malengo ya washirikina wa kale kuwaomba waungu wao

na kwamba kuwakusudia kwao Malaika, au Mitume na mawalii hakuna jengine walichokuwa wanataka isipokuwa tu maombezi yao na kujikurubisha kwa Allaah kwa hilo, ndio yaliyofanya kuhalalika damu yao na mali zao,

MAELEZO

Watu hawa hawakusema kuwa Malaika, Mitume na mawalii ambao wanawaabudu kwamba wanaumba, wanaruzuku, wanahuisha na kwamba wanafisha. Hawakusema haya. Waliwafanya tu kuwa ni waombezi wao na wakati kati baina yao na Allaah. Amesema (Ta´ala):

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Wanaabudu badala ya Allaah visivyowadhuru wala kuwanufaisha na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.”” (10:18)

Hawakutaka kutoka kwao jengine isipokuwa uombezi tu na huku wakidai kuwa huku ni kuwaadhimisha. Walikuwa wakisema kuwa Allaah ni Mkubwa na hivyo hawawezi kumfikia na kwamba wanahitaji kumchukua mja mwema, Malaika au Mtume ambaye atawafikishia haja zao. Wamemlinganisha Allaah na wale wafalme wa duniani ambao wale walio karibu nao wanawapitia mbele na kuwaombea wahitaji. Wao hawakuitakidi ya kwamba wanaumba au wanaruzuku kama wanavyosema wajinga ya kwamba shirki ni kule mtu kuamini kwamba kuna yeyote anayeumba au anayeruzuku pamoja na Allaah. Hakuna mwanaadamu yeyote mwenye busara aliyesema hivo. Walichokuwa wanalenga kutoka kwao ni uombezi. Katika Aayah nyingine imekuja:

مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ

“Na wale waliojichukulia badala Yake walinzi [husema]: “Hatuwaabudu isipokuwa ili watukurubishe kwa Allaah ukaribio.” (39:03)

Wanasema kuwa wao ni madhaifu na Allaah (Jalla wa ´Alaa) jambo Lake ni kubwa na hivyo wanamuomba kwa kupitia mkati kati na kwamba wanawakurubisha mbele ya Allaah. Wamemlinganisha Allaah na wafalme wa duniani. Huu ndio msingi wa kufuru. Inafahamisha ya kwamba hawakuitakidi kwao shirki katika uola bali walichoitakidi kwao ni shirki katika uungu.

Leo ukiwauliza wale wenye kuchinja au kuweka nadhiri kwa ajili ya makaburi ni kipi kilichowapelekea kufanya hivo? Wote watasema msemo mmoja na kuapa ya kwamba hawaitakidi kuwa wanaumba au wanaruzuku au kwamba wanamiliki kitu mbinguni au ardhini na kwamba wao wanaonelea tu kuwa ni wakati kati kwa sababu ni waja wema wawezao kumfikishia Allaah haja zao. Watasema kuwa hayo ndio malengo yao. Pamoja na hivyo Allaah amewaita kuwa ni washirikina na akamuamrisha Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupambana nao Jihaad. Amesema (Ta´ala):

فَإِذَا انسَلَخَ الْأَشْهُرُ الْحُرُمُ فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَاحْصُرُوهُمْ وَاقْعُدُوا لَهُمْ كُلَّ مَرْصَدٍ ۚ فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

“Itapomalizika miezi mitukufu, basi waueni washirikina popote muwakutapo na wachukueni [kuwafanya mateka] na wazingireni na wakalieni katika kila sehemu ya uvamizi. Lakini wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi iacheni njia yao. Hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (09:05)

Pamoja na kuwa wao wanasema kuwa hawaamini kuwa wanaumba, wanaruzuku au wanaendesha mambo pamoja na Allaah na kwamba wao walicholenga tu ni kuwafanya wakati kati. Wanasema kuwa wao wanawawekea nadhiri na wanatawasali kwao kwa kuwa Allaah hakuna chochote katika mambo yao kinachomfikia isipokuwa kwa kufanya hivo. Wanadai kuwa wao wanawafikisha kwa Allaah na wanakuwa ni wakati kati yao wenye kuwakurubisha mbele ya Allaah. Huu ndio utata wao hapo kale. Kadhalika vilevile ndio utata wa waabudu makaburi hii leo:

تَشَابَهَتْ قُلُوبُهُمْ

“Nyoyo zao zimeshabihiana.” (02:118)

Vitendo na maneno yao yamefanana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 05/11/2016