21. Makusudio ya Takfiyr ya Salaf kwa baadhi ya mapote na baadhi ya Ahl-ul-Bid´ah

Swali 21: Salaf wanapowakufurisha watu maalum wa madhehebu ya Jahmiyyah, kama ambavo ash-Shaafi´iy alivyomkufurisha Hafsw al-Fard wakati aliposema kuwa Qur-aan ni kiumbe, ambapo ash-Shaafi´iy akamwambia kuwa amemkufuru Allaah Mtukufu, kama alivyonukuu al-Laalakaa’iy katika ”Sharh Usuul I’tiqaad Ahl-is-Sunnah”, na kama walivyokafirishwa Jahm bin Swafwaan, Bishr al-Maariysiy, an-Nadhwaam na Abul-Hudhayl al-‘Allaaf, kama alivyonukuu Ibn Battwah katika ”al-Ibaanah as-Sughraa” – Je, wanakusudia kuwakufurisha watu hawa wenyewe kama wenyewe au maneno yao ndio ya kikafiri na si wao kama wao?

Jibu: Dhahiri ni kwamba kinachokusudiwa ni kuwakufurisha wao kama wao kutokana na kutajwa majina yao kwa upekee. Vivyo hivyo kinachohihiri ni kwamba ash-Shaafi´iy alimjadili na akasimamisha hoja dhidi yake. Kunapokusudiwa kukufurisha kwa ujumla ni kama pale baadhi yao wanaposema:

”Jahmiyyah ni makafiri.”

Lakini pale wanapobainishwa watu maalum waliokabiliana na maimamu na kujadiliana nao, makusudio inakuwa kuwakufurisha wao kama wao. Wanazuoni wana mitazamo tofauti kuhusu kuwakufurisha Jahmiyyah:

1 – Wako wenye kuona kuwa wale waliochupa mipaka ni makafiri.

2 – Wengine wakaona kuwa wote ni makafiri.

3 – Wengine wakaona kuwa wote ni wazushi.

Inapokuja kwa wale mmojammoja ambao waliwakabili maimamu na wakajadiliana nao, udhahiri ni kwamba waliwakufurisha wao kama wao kwa sababu hoja inakuwa imesimama dhidi yao.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 51
  • Imechapishwa: 08/01/2026