Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

43 – Hodhi ambayo Allaah (Ta´ala) atamkirimu ili iwe ni burudisho la kiu ya ummah wake ni haki.

MAELEZO

Kwa mujibu wa maimamu wengi Hadiyth zinazozungumzia Hodhi ni nyingi mno na zimefikia kiwango cha kupokelewa kwa wingi. Karibu Maswahabah thelathini na kitu wamezipokea. Haafidhw Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amezitaja zote mwishoni mwa kitabu chake ”an-Nihaayah”. Haafidhw Ibn Abiy ´Aaswim ameandika milango saba katika kitabu chake ”Kitaab-us-Sunnah”[1] kuhusu Hodhi ambapo akaashiria juu ya kupokelewa kwake kwa wingi na kusema:

”Khabari tulizotaja kuhusu hodhi yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inafidisha elimu.”

[1] Kitaab-us-Sunnah (155-161) na (697-776) kwa ukaguzi wangu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 22/09/2024