Kuhusu kuingia ndani ya maneno ya wanafalsafa, si vengine isipokuwa ni shari tupu. Ni mara chache mno mtu ataingia ndani ya chochote katika hayo isipokuwa atachafuliwa kwa baadhi ya madhara yake. Ni kama alivosema Ahmad:
“Hakuna yeyote anayetazama falsafa isipokuwa anakuwa Jahmiy.”
Yeye na wengineo katika Salaf walikuwa wakitahadharisha wanafalsafa ingawa watatetea Sunnah.
Na kuhusu ambaye anapenda falsafa iliyozuliwa na kuwafuata watetesi wake kumsimanga ambaye haingii ndani ya mizozo na mijadala na akamtuhumu ujinga, kutokuwa na thamani na kwamba si mwenye kumtambua Allaah au dini Yake, si jengine isipokuwa ni nyayo za Shaytwaan. Tunamwomba Allaah ulinzi kutokamana nayo.
- Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 69-70
- Imechapishwa: 23/09/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)