Vivyo hivyo kuhusu watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wana haki ya ule ujamaa na haki ya imani. ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kuwapenda watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusu Nawaaswib, wanawapenda Maswahabah na huku wanawachukia watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ndio maana wakaitwa hivo. Raafidhwah wao ni kinyume na hivo. Wanadai kuwa wanawapenda watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na sambamba na hilo wanawachukia, wanawalaani, kuwakufurisha Maswahabah na kuwataja kwa ubaya.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 227-228
  • Imechapishwa: 22/04/2025