Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

154 – Tunawapenda Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

MAELEZO

Swahabah ni yule ambaye amekutana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akamuamini na akafa hali ya kuwa ni muislamu. Akimuamini na asikutane naye, hazingatiwi kuwa ni Swahabah hata kama aliishi kipindi cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mfano wa watu hao ni an-Najaashiy. Isitoshe ni sharti ili azingatiwe kuwa ni Swahabah amuamini na afe hali ya kuwa ni muumini. Pale tu ataporitadi basi ubabatilika usuhuba wake na matendo yake mengine yote.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 225
  • Imechapishwa: 21/04/2025