111- Kisha siku hiyohiyo ataenda katika Ka´bah. Atatufu mara saba, kama alivyofanya siku ile alipofika. Isipokuwa tu hatoipitisha Ridaa´ yake chini ya kwapa na wala hatokwenda kwa haraka.

112- Miongoni mwa Sunnah ni yeye kuswali Rak´ah mbili katika mahali pa kusimama Ibraahiym. Haya yamesemwa na az-Zuhriy[1] na yakatendewa kazi na Ibn ´Umar[2] na akasema:

“Kila baada ya mzunguko wa saba inatakiwa kuswali Rak´ah mbili.”[3]

113- Kisha atafanya Sa´y baina ya Swafaa na Marwah kama ilivyotangulia kutajwa. Kuhusu Qaarin na Mufrid, watatosheka na ile Sa´y ya kwanza.

114- Baada ya Twawaaf hii kitahalalika kwake kila kitu kilichokuwa haramu kwake wakati wa Ihraam yake mpaka wanawake wake.

115- Ataswali Dhuhr huko Makkah. Ibn ´Umar amesema:

“Huko Minaa.”[4]

116- Ataiendea zamzam na kunywa kutoka humo.

[1] Ameipokea al-Bukhaariy kwa mlolongo wa wapokezi uliopungua wakati Ibn Abiy Shaybah na wengineo wameipokea kwa cheni ya wapokezi ilioungana. Rejea katika ”Mukhtaswar al-Bukhaariy” (1/386/319).

[2] Ameipokea al-Bukhaariy kwa mlolongo wa wapokezi uliopungua wakati ´Abdur-Razzaaq ameipokea kwa cheni ya wapokezi ilioungana. Rejea katika ”Mukhtaswar al-Bukhaariy” (1/386/318).

[3] Ameipokea ´ Abdur-Razzaaq (9012) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kutoka kwake.

[4] Allaah ndiye mjuzi zaidi ni kipi katika mawili hayo alichokuwa akifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Inawezekana aliswali pamoja nao mara mbili; siku moja wapo Makkah na siku nyingine Minaa. Hiyo ya kwanza ilikuwa ni faradhi na hiyo ya pili ilikuwa ni sunnah. Kitu kama hicho alikifanya katika baadhi ya vita vyake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 20/07/2018