Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

… na ukaelewa dini ya Allaah ambayo amewatuma kwa ajili yake Mitume, kuanzia wa mwanzo wao mpaka wa mwisho wao, ndio dini pekee ambayo Allaah anaikubali kutoka kwa mtu, na ukafahamu jambo ambalo limekuwa halitambuliki kwa watu wengi kutokana na hili, utapata faida mbili…

MAELEZO

Maneno yake mtunzi (Rahimahu Allaah):

” … na ukaelewa dini ya Allaah ambayo amewatuma kwa ajili yake Mitume… “

Nayo ni kumwabudu Allaah pekee. Amesema (Ta´ala):

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Na Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana muabudiwa wa haki ila Mimi; hivyo basi Niabuduni.”” (21:25)

Huu ndio Uislamu ambao Allaah amesema juu yake:

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ

“Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu, basi haitokubaliwa kwake.” (03:85)

Maneno yake mtunzi (Rahimahu Allaah):

” … na ukafahamu jambo ambalo limekuwa halitambuliki kwa watu wengi kutokana na hili… “

Bi maana maana ya matamshi haya ambayo mtunzi wa kitabu ametangulia hapo kabla kuitaja pindi aliposema:

“Ukishajua ya kwamba makafiri wajinga walijua hilo, jambo la kushangaza ni kwa yule anayedai Uislamu na yeye hajui maana ya neno hili… “

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kash-ish-Shubuhaat, uk. 43-44
  • Imechapishwa: 14/10/2023