Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kula au kunywa mchana wa Ramadhaan kwa kusahau?

Jibu: Hakuna neno juu yake na swawm yake ni sahihi. Allaah (Subhaanah) amesema mwishoni mwa Suurah “al-Baqarah”:

رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1]

Imesihi kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kwamba Allaah (Subhaanah) amesema:

“Nimefanya hivo.”

Pia imethibiti kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kusahau ambapo akala au akanywa basi aikamilishe swawm yake. Kwani si vyengine Allaah ndiye kamlisha na kumnywesha.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] 02:286

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ashyaa´ laa tufsid-is-Swawm, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 03/04/2021