20. Kitu cha kwanza kinachomsaidia mwanamke kuwa mwema

6 – Mambo yanayomsaidia mke kupata sifa hizi

1 – Kutambua ukubwa wa Allaah (Ta´ala), kwamba Yeye ni wa haki na Mwenye kukisimamia kila kitu, dini Yake ndio mfumo imara, Shari´ah Yake ndio njia ilionyooka, kutambua ukamilifu wa hekima Zake katika maamrisho na makatazo Yake na mipango na matakwa Yake. Vilevile kutambua kuwa ujuzi Wake umekienea kila kitu chenye kuonekana na kilichojificha. Hakika Yeye anayajua yanayowanufaisha waja kutokamana na yanayowadhuru, yenye kuwafanya wakatengemaa na yenye kutokamana na yenye kuwaharibu. Hakika Yeye (Subhaanah) ni Mwingi wa wenye huruma. Hawaamrishi waja Wake isipokuwa katika yaliyo na manufaa katika dini na dunia yao na kuwafanya wakafaulu duniani na Aakhirah. Kama ambavo hawakatazi isipokuwa yale yenye kuwafanya wakaangamia duniani na Aakhirah.

Kwa hiyo Shari´ah Yake (Subhaanah) ndio rehema, kheri na baraka. Yeyote atakayeifuata basi atafaulu duniani na Aakhirah na ataishi maisha ya starehe na mazuri yaliyojaa furaha. Kwa msemo mwingine hatopata maangamivu wala dhiki kabisa isipokuwa pindi atakapokwenda kinyume na maamrisho ya Bwana Wake (´Azza wa Jall). Allaah (Ta´ala) amesema:

مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Yule mwenye kutenda mema katika wanamme au wanawake – ilihali ni muumini – basi Tutamhuisha maisha mazuri na tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.”[1]

وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ

“Yeyote atakayejitenga na ukumbusho Wangu, basi hakika atapata maisha ya dhiki[2] na tutamfufua siku ya Qiyaamah hali ya kuwa kipofu.”[3]

Hivyo basi, mke akijua kiwango hichi cha utukufu wa Allaah (Ta´ala) na ukamilifu wa hekima, kuenea kwa ujuzi Wake, ukunjufu wa rehema Zake, basi atakimbilia kumtii (Jalla wa ´Alaa) na yale aliyoamrisha kuhusu kumtii mume Wake, atakimbilia kutekeleza haki zake pasi na kusita wala kufanya uvivu na wala hatoanza kuhoji ni kwa nini mwanamme amefanywa kuwa ni msimamizi juu yake, ni kwa nini nimelazimishwa kumtii na kadhalika? Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا

“Anayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi hakika amepotoka upotofu wa wazi.”[4]

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana kati yao kisha wasipate katika nyoyo zao uzito katika yale uliyohukumu na wajisalimishe kwa kujisalimisha.”[5]

[1] 16:97

[2] Dhiki, shida na majanga. Ameyaelezea maisha kuwa yenye majanga mno kwa njia ya kupetuka. (Waabil as-Swayyib, uk. 59)

[3] 20:124

[4] 33:36

[5] 04:65

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 37-39
  • Imechapishwa: 03/10/2022