Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Mambo yanayochengua wudhuu´ ni manane:
1 – Kila kinachotoka kupitia tupu ya mbele au ya nyuma.
2 – Kila kichafu au najisi inayotoka kwenye mwili.
3 – Kutokwa na akili.
4 – Kumgusa mwanamke kwa matamanio.
5 – Kugusa tupu ya mbele au ya nyuma kwa mkono.
6 – Kula nyama ya ngamia.
7 – Kuosha maiti.
8 – Kuritadi kutoka katika Uislamu – Tunamuomba Allaah atukinge na hilo.
MAELEZO
1 – Kichenguzi cha kwanza cha wudhuu´: Ni kila kinachotoka kupitia njia mbili za haja kubwa na ndogo. Na ni kitu chochote kinachotoka humo, ni mamoja iwe ni kinyesi, mkojo, upepo, damu, manii, madhiy au kinginecho. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Allaah hapokei swalah ya mmoja wenu anapopatwa na hadathi mpaka atawadhe.”
Ameipokea al-Bukhaariy (6954) na Muslim (537) kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 21-22
- Imechapishwa: 25/05/2026
Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Mambo yanayochengua wudhuu´ ni manane:
1 – Kila kinachotoka kupitia tupu ya mbele au ya nyuma.
2 – Kila kichafu au najisi inayotoka kwenye mwili.
3 – Kutokwa na akili.
4 – Kumgusa mwanamke kwa matamanio.
5 – Kugusa tupu ya mbele au ya nyuma kwa mkono.
6 – Kula nyama ya ngamia.
7 – Kuosha maiti.
8 – Kuritadi kutoka katika Uislamu – Tunamuomba Allaah atukinge na hilo.
MAELEZO
1 – Kichenguzi cha kwanza cha wudhuu´: Ni kila kinachotoka kupitia njia mbili za haja kubwa na ndogo. Na ni kitu chochote kinachotoka humo, ni mamoja iwe ni kinyesi, mkojo, upepo, damu, manii, madhiy au kinginecho. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Allaah hapokei swalah ya mmoja wenu anapopatwa na hadathi mpaka atawadhe.”
Ameipokea al-Bukhaariy (6954) na Muslim (537) kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 21-22
Imechapishwa: 25/05/2026
https://firqatunnajia.com/20-kila-kinachotoka-kupitia-tupu-ya-mbele-au-ya-nyuma/