21. Kila kichafu au najisi inayotoka kwenye mwili

2 – Kichenguzi cha pili cha wudhuu´: Kila kichafu au najisi inayotoka kwenye mwili. Wanazuoni wametofautiana kuhusu damu inayotoka kwa njia isiyo ya haja kama inabatilisha wudhuu´ au hapana. Baadhi ya wanazuoni wameona kuwa haibatilishi wudhuu´ kwa sababu hakuna chochote kilichothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu hilo. Wanazuoni wengine wakaona kuwa wudhuu´ unabatilika ikiwa damu hiyo ni nyingi na inachukiza, jambo ambalo limenukuliwa kutoka kwa baadhi ya Maswahabah na wanafunzi wao. Nalo ndilo alilolichagua Shaykh (Rahimahu Allaah) hapa. Aidha kufanya hivo ni kuchukua kilicho na tahadhari na kutoka nje ya tofauti. Tazama ”al-Mughniy” (1/247) na ”Majmuu´-ul-Fataawaa” ya Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) (10/159) na ”Fataawaa al-Lajnah ad-Daa’imah” (5/261).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 25/05/2026