5- Miongoni mwa vifunguzi ni kujitapisha. Kitu kama hicho kinamfunguza mfungaji. Ama matapishi yakimzidi na yakatoka pasi na kutaka kwake, kitu hicho hakiathiri funga yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ambaye yatamshinda matapishi hakuna juu yake kulipa na ambaye atajitapisha basi alipe.”[1]

Maana ya maneno:

“… yatamshinda matapishi… “

ni kwamba yametoka pasi na kutaka kwake.

Maana ya maneno:

“… ambaye atajitapisha… “

ni kwamba amefanya makusudi kujitapisha.

[1] Abu Daawuud (2380), at-Tirmidhiy (719) na Ibn Maajah (676).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/384)
  • Imechapishwa: 04/04/2021